ZAHERA AWATULIZA YANGA

NA TIMA SIKILO

USITISHIKE na Yanga kulazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Zesco United nyumbani.Hivi ndivyo Kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera amewaambia mashabiki kwa kusema watulize mzuka kwani kikosi chake kitapindua meza kibabe mechi ya marudiano huko Zambia.
Yanga jana ililazimishwa sare na Zesco mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo Zahera alisema,matokeo hayo hayamtishi kwani anaamini vijana wake wanaweza kufanya makubwa ugenini kama kilichowakuta Township Rollers ya Botswana.
“Matokeio haya hayanitishi kama wao wameweza kutumbukiza goli kwetu hata na sisi tuna uwezo mkubwa wa kufanya hivyo kwao,kitu kikubwa kwetu tunakwenda kujipanga na mchezo ujao,”alisema Zahera.
Katika mchezo huo Yanga walitangulia kwa bao la mkwaju wa penalti likiwekwa wavuni na kiungo wake mshambuliaji, Patrick Sibomana dakika ya 24 akimchambua kipa Jacob Banda.
Refa wa pambano hilo Helder Martin Rodriguez alitoa penalti hiyo baada ya Marcel Kalonda kumchezea rafu Mnamibia wa Yanga, Sadney Urikhob.
Kuingia kwa bao hilo kuliwafanya Yanga kupanga mashambulizi ya kutafuta bao la pili lakini Zesco wakaka imara kuzipa mianya huku nao wakifanya mashambulizi ya kushtukiza.
Hadi dakika 45 za kwanza zinaisha Yanga walitoka wakiongoza kwa bao hilo.Kipindi cha pili kilianza tena kwa kasi kwa timu zote kushambuliana kwa zamu ambapo Yanga walikosa mabao ya wazi kupitia kwa Sibomana dakika ya 48, Mapinduzi dakika ya 52 pamoja na Tshishimbi dakika ya 53.
Zesco walisawazisha bao hilo dakika za majeruhi kupitia kwa kiungo wa zamani wa Yanga Thaban Kamusoko aliyeachia mkwaju ulitiotinga moja kwa moja nyavuni na kufanya machezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Timu hizo zitarudiana Septemba 27 huko Zambia uwanja wa Levi Mwanawasa na ili isonge mbele inapaswa kuibuka na ushindi wa aina yoyote.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata, Mapinduzi Balama/Ali Ali dk74, Ally Mtoni ‘Sonso’, Lamine Moro, Kelvin Yondan, Feisal Salum, Mohammed Issa ‘Banka’/Mrisho Ngassa dk58, Abdulaziz Makame, Papy Kabamba Tshishimbi, Sadney Urikhob/Maybin Kalengo dk58 na Patrick Sibomana.
Zesco United; Jacob Banda, Marcel Kalonda, Simon Silwimba, Anthony Akumu, John Ching’andu/Kondwani Mtonga dk64, Kasumba Uma


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*