Taifa Stars watua salama Kigali

NA TIMA SIKILO

KIKOSI cha Tanzania, Taifa Stars, kimetua salama nchini Rwanda, tayari kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya wenyeji utakaochezwa Jumatatu ijayo mjini Kigali.

Akizungumza na BINGWA jana, Kaimu Kocha Mkuu wa Stars, Ettiene Ndayiragije, alisema wamepokewa mazuri, licha ya kuwapo kwa mvua kubwa inayoendelea kuonyesha nchini humo.

Ndayiragije alisema baada ya kuwasili walitarajia kufanya mazoezi jana jioni kutegemea na hali ya hewa ya Rwanda. 

“Tunamshukuru Mungu tumefika salama, ingawa kuna mvua kubwa inanyesha, lakini haitaathiri utendaji kazi wetu,” alisema Ndayiragije

Alisema mchezo huo, utampa maandalizi mazuri kuelekeza pambano lao la marudiano la kuwania kufuzu michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi ya Ndani (CHAN) dhidi ya Sudan uliopangwa kuchezwa Oktoba 18, mwaka huu, kwenye Uwanja wa El-Merreikh Omdurman.

Taifa Stars inahitaji ushindi wa mabao 2-0, baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa hivi karibuni kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, kufungwa bao 1-0.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*