googleAds

Sven apata dawa ya Kagere

NA WINFRIDA MTOI

BAADA ya mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, kuonekana amepunguza kasi katika upachikaji wa mabao na tayari kocha wa timu hiyo, Sven Vandenbroeck, amepata dawa ya kumfanya aweze kufunga zaidi ya matatu yaani Hat-Trick.

Licha ya Kagere kuongoza katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara,lakini kasi yake imepungua tofauti na msimu uliopita aliochukua kiatu cha dhahabu kwa kutupia mabao 23.

Hata hivyo, Kagere anaonekana kushindwa kufunga kama ambayo timu hiyo ilivyokuwa ikifundishwa na Patrick Aussems kabla ya ujio wa Vandenbroeck aliyekuja na mfumo mpya wa uchezaji.

Vandenbroeck  amekuwa akitumia kuchezesha mshambuliaji mmoja mbele, jambo lilolofanya Kagere kuwa na pacha wa kumlisha mipira kama ambavyo Aussems alikuwa anatumia mfumo wa kuchezesha washambuliaji wawili mbele.

Baada  ya kubaini tatizo la Kagere, lakini timu kushindw kupata mabao mengi, amerejesha mfumo wa kuwatumia washambuliaji wawili mbele na sasa Kagere atakuwa anasimama na John Bocco.

Mfumo wa kuchezesha washambuliaji wawili ulianza kumpa matunda mazuri katika  mchezo uliopita ambao walishinda mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Katika mchezo huo, Bocco ndiye alifunga bao la kwanza kutokana na kazi nzuri aliyofanya Kagere,kwani wawili hao wakicheza pamoja kasi ya ushambuliaji inakuwa kubwa.

Hata hivyo, Sven alikiri kuwa mfumo wa 4:4:2 alioanza kuutumia kwa kumwanzisha Kagere na Bocco pamoja umekuwa na mafanikio.

“Pacha ya Bocco na Kagere wakicheza  pamoja inafanya timu kuwa na uwezo mkubwa wa kupeleka mashambulizi mbele, nina imani tutafunga mabao mengi zaidi kama itaendelea hivi,” alisema.

Previous Article

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*