STRAIKA SAUDI ARABIA KUJIFUA MAN UNITED

MANCHESTER, England

IKIWA ni sehemu ya maandalizi ya fainali za Kombe la Dunia, straika wa timu ya Taifa ya Saudi Arabia, Mohammad Al-Sahlawi, atafanya mazoezi na kikosi cha Manchester United.

Al-Sahlawi mwenye umri wa miaka 31, ameshafunga mabao 26 katika mechi 33 alizoichezea Saudi na timu yake hiyo itakuwa Urusi mwaka huu kucheza fainali hizo zitakazoanza Juni 14, mwaka huu.

“Imeshakubaliwa na Manchester United kuwa Mohammed Al-Sahlawi, atajiunga na programu ya mazoezi kwa wiki tatu,” ilisema taarifa kutoka Saudi.

Hata hivyo, imewekwa wazi kuwa hakuna mpango wowote wa Man United kutaka kumsajili Al-Sahlawi, ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akikosolewa kwa kushuka kiwango.

Wakati huo huo, Man United wameripotiwa kupeleka ofa nono ya pauni milioni 42 kwa Bayern Munich, ili kuwashawishi kumwachia kiungo wao, Arturo Vidal.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*