Simba, Yanga Princess kukutana Desemba 14

NA ZAINAB IDDY

NA MWANDISHI WETU

TIMU ya Simba Queens imepangwa kucheza na Yanga princess katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara utakaochezwa Desemba 14, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Karumbe, Dar es Salaam. 

Ligi hiyo ambayo itaanza Oktoba 26, mwaka huu, Simba Queens itafungua dimba na Ruvuma Queens kwenye Uwanja Karume, Dar es Salaam.

Mchezo mwingine, utakuwa kati ya wenyeji Tanzanite na Yanga Princessutakaochezwa kwenye Uwanjawa Sheikhe Amir Abeid, mkoani Arusha, wakati Alliance Girls itakuwa kucheza na Kigoma Sisters.

Timu ya Mlandizi Queens itakuwa na kibarua kigumu watakapomenyana na Panama  kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani  na Baobab Queens watavaana na mabingwa watetezi wa ligi hiyo, JKT Queens.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*