Rayvanny kwenye kollabo na msanii wa Jay Z

NA JESSCA NANGAWE

STAA kutoka lebo ya WCB Raymond Mwakyusa maarufu Rayvanny yupo mbioni kuachia ngoma yake mpya akiwa kamshirikisha msanii aliyewahi kufanya kazi chini ya lebo ya rapa mkubwa dunia Jay Z.
Huu ni mfululizo wa msanii huyo kufanya kazi na wasanii wakubwa nje ya Tanzania akiwepo Pitbull, Jasonderulo na Norafatehi wote kutoka Marekani.
Akizungumza na DIMBA, Rayvanny alisema yupo kwenye maandalizi ya mwisho kuachia ngoma hiyo kupitia lebo ya Rock Nation na msanii huyo anayejulikana kwa jina la Philly.
“Naamini ni mwendelezo wangu wa kufanya kazi na wasanii wakubwa, lengo ni kuufikisha muziki wa Bongofleva mbali zaidi, haya yote ni mafanikio ambayo nazidi kuyapata kutokana na ubora wa kazi zangu”alisema Rayvanny .


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*