Ozil apata mtoto wa kike

LONDON, England

KIUNGO wa Arsenal, Mesut Ozil, ametuma picha ya mtoto wake wa kwanza wa kike katika ukurasa wa instagram baada ya kuzaliwa. Picha hiyo iliambatana na maneno ya furaha ya kumshukuru Mungu kwa baraka hiyo katika familia yake.

“Asante Mungu mtoto wangu amezaliwa kwa afya tele, nakuomba utuongoze katika hili jema,” aliandika Ozil. Ozil alimuoa mpenzi wake wa muda mrefu Gulse, mwaka jana nchini Uturuki. Pierre-Emerick Aubameyang, Alexandre Lacazette, Shkodran Mustafi, walikomenti salamu za pongezi kwa mchezaji mwenzao.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*