MWAKYEMBE AFUTA ADHABU YA ROMA, PRETTY KIND

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, jana alitengua adhabu ya kutofanya sanaa kwa miezi sita waliyopewa wasanii wa Bongo Fleva, Ibrahim Musa ‘Roma Mkatoliki’ na Suzan Michael ‘Pretty Kind’, kwa makosa ya kukiuka maadili katika kazi zao.

Akizungumza na waandishi wa habari katika  mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana kwenye ofisi za Wizara hiyo, Naibu Waziri Juliana Shonza, alisema wasanii hao walikiri makosa yao mbele ya Waziri Dk. Mwakyembe na Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza, hivyo hawana budi kusamehewa na kuwa mabalozi wa maadili.

“Suzan (Pretty Kind) amejirekebisha na yupo tayari kuwa balozi wa maadili kwa kufanya kazi zenye maadili na amekwenda mbele zaidi kwa kusajiliwa na Basata,” amesema Shonza.

Akizungumza suala la Roma, Waziri Mwakyembe alisema : “Roma amesema hataki tena huo wimbo, hatuna sababu nyingine mimi na wewe Naibu Waziri zaidi ya kumsamehe, kimebaki kipengele kimoja cha kusajiliwa na Basata, siku atakapokabidhiwa cheti chake cha usajili na Basata ndipo adhabu yake itakuwa imekwisha”.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*