Makame, Balama tema mate chini

NA MAREGES NYAMAKA

KIWANGO cha nyota wawili wa Yanga, Abdulazizi Makame sambamba na Balama Mapinduzi katika mchezo wao jana Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya Zesco kilikuwa bora zaidi kuliko mchezaji yeyote wa timu hiyo.

Makame hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika alikuwa amepiga pasi sahihi 69 zote zikimfikia mlengwa, na kutengeneza nafasi mbili ambazo hazikutumiwa vema na wenzake kuweka mpira kimiani.

Kama hiyo haitoshi nyota huyo ambaye alicheza sambamba na pacha wake Feisal Salum Toto alikuwa amepokonya mpira kwa adui mara tano huku yeye akipoteza mara sita.

Kwa upande wa Balama Mapinduzi ambaye alibadilishiwa majukumu kucheza beki wa kulia alionekana kuitendea haki nafasi hiyo kabla ya kuumia kipindi cha pili.

Ingizo hilo jipya kutoka Alliance akifanikiwa kuokoa hatarishi mpira ukielekea langoni alifanya hivyo mara tatu lakini pia akikokota mpira mara saba.

Hadi anaumia nafasi yake inachukuliwa na Ali Ali alikuwa amefumua mashuti mawili langoni ingawa hayakulenga lango na kutengeneza nafasi mbili ambazo hazikutumiwa vema.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*