Lukaku aweka rekodi Ubelgiji

BRUSSELS, Ubelgiji

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Romelu Lukaku, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufikisha jumla ya mabao 50 na zaidi akiitumikia taifa hilo.

Lukaku alifunga mabao mawili na kutengeneza moja katika ushindi mnono wa 9-0 dhidi ya San Marino na kufanya Ubelgiji kuwa timu ya kwanza kufuzu michuano ya Mataifa ya Ulaya (EURO) zitakazofanyika mwakani.

Straika huyo aliyetua Inter Milan baada ya kutemwa na Manchester United amefikisha mabao 51 katika mechi 83 alizocheza akiwa na timu ya taifa. 

Katika mechi zote saba ambazo Ubelgiji imecheza katika Kundi I kufuzu Euro 2020, hawajapoteza mchezo hata moja huku wakiruhusu bao moja tu.

Timu zingine mbali na Ubelgiji na San Marino katika Kundi I ni Scotland, Kazakhstan, Cyprus na Urusi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*