Linah sasa ni anga za Dubai tu

NA JESSCA NANGAWE

MREMBO kutoka kiwanda cha Bongofleva Lina Sanga anatarajia kufanya shoo ya aina yake katika nchi za Falme ya Kiarabu Novemba 15 mwaka huu.
Akizungumza na DIMBA,Linah alisema, moja ya michongo yake mwaka huu ni kwenda kutumbuiza Duba na kwingineno duniani ambako aanaendelea kunusa dili.
“Nashukuru kazi zangu zimezidi kunitambulisha kama msaniii mkubwa, kwa sasa nina ofa karibu tatu lakini kwa kuanza ni hii shoo ambayo itafanyika Novemba 15 nchini Dubai na baada ya hapo nitaendelea na nyingine,”alisema Linah.
Alisema anafurahi kuona mashabiki zake wakiendelea kusapoti kazi zake ambazo zinaendelea kumpa michongo sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
Linah kwa sasa anafanya vyema na ngoma yake mpya ya Nimenasa aliyoshirikiana na msanii mwenzake Amin.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*