LADY JAY DEE, MWANA FA KUWEKA HISTORIA ANAWEZA CONCERT

NA CHRISTOPHER MSEKENA

KUELEKEA onyesho la Anaweza Concert, litakalofanyika kesho katika Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam, wakongwe wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ na Hamis Mwinjuma (Mwana Fa), wanatarajia kukata kiu ya burudani kwa mashabiki zao baada ya kumaliza bifu lao la muda mrefu.

Itakumbukwa kuwa Juni 14, mwaka 2013, waliandaa maonyesho yao mawili yaliyoshinda na yaliyochochea ugomvi wao, baada ya Lady Jay Dee kufanya onyesho la kutimiza miaka 13 ya kuwapo kwenye muziki katika ukumbi wa Nyumbani Lodge, huku Mwana Fa akifanya onyesho la The Fainest, lililofanyika Makumbusho, Posta.

Kutoka hapo wawili hao wakawa maadui kufikia hatua ya Lady Jay Dee kuondoka kwenye mahojiano fulani aliyofanyiwa baada ya kuulizwa swali kuhusu Mwana Fa.

Ugomvi wao ulimalizika mwaka jana, baada ya kufanya mazungumzo binafsi na Mwana Fa kuonyesha sapoti kwa Lady Jay Dee kuutangaza wimbo wake wa I Miss You.

Mwana Fa na Lady Jay Dee wanasubiriwa kwa hamu kutumbuiza nyimbo zao zilizowahi kufanya vizuri kama vile Usiache Kuongea, Hawajui, Alikufa kwa Ngoma na Sikiliza walioshirikishwa na marehemu Ngwea.

Mbali na wakongwe hao, onyesho la Anaweza litapambwa na mastaa wengine kama vile Bushoke, Nikki Mbishi, Domokaya, Alawi Jr na wasanii wengine


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*