googleAds

Kocha Ruvu Shooting haamini kilichomtokea

ZAINAB IDDY

KOCHA Mkuu wa Ruvu Shooting, Abdulmutik Haji, alisema kuwa hadi sasa bado hajaamini kama kikosi chake kimesalia katika Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na hali mbaya waliyokuwa nayo.

Ruvu Shooting imefanikiwa kusalia katika ligi hiyo baada ya kumaliza ikiwa nafasi ya 15 kwa kuvuna pointi 45, sawa na Mbao FC iliyopo nyuma yake.

Akizungumza na BINGWA, Haji alisema kutokana na changamoto alizokutana nazo ndani ya msimu mzima,  alikuwa  amekata tamaa, lakini mechi ya mwisho ikawaokoa.

 “Ni ngumu kuamini, ila mwisho wa siku namshukuru Mungu kwa kutupigania na kutupa nafasi nyingine ya kushiriki Ligi Kuu msimu ujao, tutapambana ili tusipate matatizo kama yaliyotukumba.

“Changamoto zilichangiwa na jinsi ligi ilivyoendeshwa, kwani hakukuwa na usawa, waamuzi nao hawakuwa sawa, miundombinu na kutuweka katika hali mbaya kwenye msimamo.”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*