Kocha Nigeria aachia ngazi

LAGOS, Nigeria 

KOCHA wa timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria maarufu Super Falcon, Thomas Dennerby, amekitema kikosi hicho licha ya kubakiza mkataba wa mwaka mmoja.

Imeripotiwa kocha huyo hana mawasiliano mazuri na Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF).

Dennervy amekwepa kuhudhuria mkutano wa usuluhishi kuondoa tofauti zao lililoandaliwa na serikali ya nchi hiyo.

NFF wamekubaliana na maombi ya Dennervy kusitisha mkataba na wameanza mchakato wa kusaka kocha mpya wa Super Falcon.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*