Kocha KMC apania kuitafuna Mbao FC

NA GLORY MLAY

KOCHA wa KMC, Etienne Ndayiragije, amesema wamejipanga kuitafuna Mbao FC ili kupata ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Akizungumza na BINGWA jana, Ndayiragije, alisema anafahamu ugumu wa Uwanja wa CCM Kirumba, lakini ameandaa jeshi lake kukabiliana na hali yoyote.

Alisema kuelekea mchezo huo, wamefanya maandalizi ya kutosha na wachezaji wake wapo kwenye hali nzuri ya kiushindani, hivyo wamepania kushinda.

Alisema Mbao FC anaifahamu na anazijua mbinu zao hivyo anaamini wachezaji wakiwa makini na kutuliza akili, itakuwa rahisi kwao kupata matokeo ya haraka.

“Hatuna wasiwasi kikosi changu kipo tayari kwenda kuvuna pointi tatu Mbao FC, tunajua kuwa michezo ya lala salama inakuwa migumu lakini tutajituma ili tuweze kufikia malengo yetu,” alisema.

KMC inashika nafasi ya nne kwa kujikusanyia pointi 49, baada ya kucheza michezo 36, kushinda michezo 11, kutoka sare michezo 16 na kufungwa michezo tisa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*