Kiiza kurudi Yanga

NA ZAINAB IDDY

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Mganda Hamis Kiiza ‘Diego’, amesema anatamani kurudi katika kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kiiza aliyeitumikia Yanga katika msimu minne Ligi Kuu Bara kuanzia 2011/12 kabla ya 2015/16 kutua Simba, imeelezwa bado anauwezo wa kucheza soka ya ushindani.

Akizungumza na BINGWA jana kwa njia ya mtandao kuwa, Kiiza alisema  bado anaikumbuka Tanzania hususan klabu ya Yanga kutokana na upendo wa mashabiki wake.

“Hadi sasa nimecheza katika timu tisa tangu nianze soka la ushindani, lakini kote huko siwezi kuisahau Yanga ambayo ndio iliyonifanya nitambulike sehemu kubwa duniani.

“Bado nacheza mpira, sina mpango wa kustaafu hivi karibuni  mipango yangu siku moja nirudi Tanzania kucheza timu ya Yanga kutokana na sababu mbalimbali, kubwa ni jinsi wanavyothamini wachezaji wao katika hali zote,” alisema.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*