Katwila awapa maneno matamu Mtibwa Sugar

NA WINFRIDA MTOI

KOCHA wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila, ameahidi timu hiyo itafanya vizuri, licha ya kuanza vibaya katika michezo mitano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katwila amerejea Mtibwa Sugar jana, alitokea Uganda ambako alikuwa na timu ya Tanzania Bara chini ya umri wa miaka 20, Ngorogoro Heroes iliyoshiriki michuano ya Chalenji na wao kuchukua ubingwa kwa kuifunga Kenya bao 1-0.

Akizungumza na BINGWA jana, Katwila, alisema wachezaji mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Ndanda utakaochezwa Oktoba 19, Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mkoani Mtwara.

“Kukosekana kwangu si sababu, matokeo tuliyopata katika mechi zilizopita ni kawaida soka, niwatoe hofu wapenzi wa Mtibwa Sugar, timu itakaa vizuri, ushindi utaanzia Mtwara,” alisema Katwila.

Katwila alisema atumia muda wiki moja uliobaki kabla ya kukutana na Ndanda kukiandaa kikosi chake ili kuweze kupata ushindi.

Alisema kabla ya kuivaa Ndanda anahitaji kupata mchezo wa kirafiki ili kuangalia upungufu na kufanya marekebisho bbaada ya kucheza michezo mitano ya ligi hiyo bila kupata pointi zote tatu.

Mtibwa Sugar inashika nafasi ya 19 katika msimamowa ligi hiyo kutokana na pointi mbili, baada ya kupata sare mbili na kufungwa michezo mitatu. 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*