KANYE AANDAMANA KUPINGA UMILIKI WA BASTOLA

WASHINGTON, Marekani

RAPA Kanye West juzi aliungana na maelfu ya waandamanaji kupinga umiliki holela wa bastola nchini Marekani.

Maandamano hayo yaliyopachikwa jina la ‘March for Our Lives’, yalifanyika mjini Washington.

Kanye hakuwa peke yake bali aliambatana na mkewe, Kim Kardashian na mtoto wao wa kike, North West.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa Kanye kuonekana katika matukio yanayohusiana na siasa tangu mwaka juzi alipomtembelea Rais  Donald Trump.

Mbali ya kuandamana, pia kulikuwa na ‘show’ kali kutoka kwa wanamuziki Ariana Grande, Miley Cyrus, Common na Vic Mensa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*