googleAds

JKT Tanzania yaikamia Mtibwa Sugar

NA ASHA KIGUNDULA

BAADA  ya kupata sare ya bao 1-1 na Lipuli katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, Kocha wa timu ya JKT Tanzania,  Mohamed Abdallah Baresi, amesema wamejipanga kuondoka na pointi zote tatu dhidi ya Mtibwa Sugar.

JKT  Tanzania wanatarajiwa kucheza na Mtibwa Sugar katika mchezo utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa wenye Uwanja wa Gairo,mkoani Morogoro.

Akizungumza na BINGWA jana, Baresi alisema anafahamu mchezo huo utakuwa ni mgumu kutokana na wapinzani wao  hawatakubali kupoteza kwa mara nyingine baada ya kufungwa na Simba mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro .

Bares alisema Mtibwa Sugar ni kati ya timu mzuri Ligi Kuu Bara, inayoweza kupambana na kupata matokeo bora.

Alisema katika mchezo wa kesho wanahitaji pointi tatu ili wafikie malengo yao ya kumaliza nafasi tano za juu katika msimamo wa ligi hiyo.

Baresi alisema timu yake iliweka kambi maalum mkoani Iringa, baada ya kumaliza kwa  mchezo wao dhidi ya Lipuli na wanakwenda Gairo kutafuta ushindi.

“Tupo katika mazoezi ya mwisho kabla ya kuanza safari ya kwenda Gairo, kwa pambano letu na Mtibwa, tunaijua Mtibwa ni timu nzuri,lakini tumejipanga kupata pointi tatu kwenye  uwanja wao wa nyumbani,”alisema Baresi.

JKT Tanzania inashika nafasi ya saba  kutokana na pointi 31, baada ya kucheza michezo 21, ikishinda  nane,  sare saba na kupoteza sita huku Mtibwa  ikiwa ya 14 kwa pointi 21, wakifungwa michezo 10,sare sita na kushinda mitano.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*