googleAds

Harmonize afuturisha mastaa Dar

NA JEREMIA ERNEST

VIONGOZI wa Serikali na watu mbalimbali maarufu nchini jana walishiriki kwenye mwaliko wa futari iliyoandaliwa na staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’, katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Harmonize aliwashukuru wadhamini wa futari hiyo Kampuni ya Bima ya Resolution kwa kuwezesha pia watu mbalimbali ambao walipenda kushiriki ila kutokana na mipangilio alichagua baadhi ya wawakilishi.

“Nilitamani nikutane na wadau wangu wote lakini kwa mwaka huu nilichagua baadhi ya wawakilishi, wakati mwingine nitajitahidi kutanua wigo zaidi hasa kwa mashabiki zangu na watu wenye mahitaji maalumu,” alisema Hamonize.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*