Guardiola ampa Aguero mbinu mpya

MANCHESTER, England 

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amemfundisha mashambuliaji wake, Sergio Aguero, namna ya kuwachenga na kuwatoka mabeki katika eneo la hatari.

Guardiola alimwalika Aguero katika chakula cha usiku, kwenye mgahawa mmoja jijini Manchester kwa lengo la kuwa naye karibu.

Imeripotiwa Guardiola ameuponda uchezaji wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina kwa siku za hivi karibuni.

Allipouliuzwa Aguero kuhusu suala hilo, alikiri kukutana na kocha wake kuzungumzia mambo mabalimbali ikiwamo falsafa zake kwenye timu.

“Kocha aliniambia nijaribu kucheza tofauti, sio rahisi lakini sina chaguo, nitamwonyesha na kujitahidi kucheza anavyotaka kwa sababu tangu nitue Man City, kila kitu kimebadilika,” alisema Aguero.

Aguero ameshikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa Man City wa muda mrefu na tegemeo katika kikosi hicho.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*