Gigy Money ajipa majukumu yote kwa Myra

NA JESSCA NANGAWE


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford maarufu ‘Gigy Money’ amesema kuwa kwasasa yeye ndiye mama na baba wa mtoto wake, Na haoni ugumu wowote kulea mwenyewe.

Akizungumza Gigy alisema kutokana na baba wa Mtoto wake kujiweka kando yeye ameamua kubeba majukumu yote na haoni tatizo hilo kwa kuwa anamudu kumlea mwanaye na kumpatia kila kitu.
Aliongeza kuhusu mahusiano yake alisema kuwa kwasasa amejifunza na kamwe hawezi kuachika achika hovyo kwa kuwa tayari amepitia achangamoto nyingi kwenye mahusiano yake ya nyuma.
“Natafuta pesa kwa ajili ya binti yangu, kwa sas amimi9 ndo baba na mama kwa mwanangu, simfikirii mtu yoyote katika malezi ya mwanangu, nimepitai changamoto nyingi za mahusiano na kwa sas ahazinipi tabu yoyote”Alisema Gigy.

Kuhusu muziki, Gigy Money alisema yeye huwa hakosei kutengeneza ngoma kali, Kwani mpaka sasa hivi hakuna msanii yeyote Tanzania, Mwenye uwezo wa kutengeneza hit song kama wimbo wake wa ‘Papa’.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*