googleAds

Four Ways mabingwa Castle Africa 5 aside

NA MWANDISHI WETU

TIMU Four Ways Fark FC ya Kinondoni, Dar es Salaam, imeibuka mabingwa katika bonanza la soka  lililofanyika juzi, kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama.

Bonanza hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Castle Lager, ambapo mshindi alizawadiwa kikombe, medali za dhahabu na Sh 1,500,000, katoni ya bia ya Castle Lager.

Pia mshindi wa bonanza hilo ataiwakilisha nchi katika fainali za Caslte Africa 5s zinazotarajiwa kufanyika mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Four Ways Park walitwaa ubingwa huo baada ya kupata pointi saba wakifuatiwa na Jacks Pub waliopata pointi nne na kuzawadiwa medali za shaba, katoni ya bia ya Castle Lager na Sh 900,000.

 Mshindi wa tatu katika fainali hizo ni Meeda Night Club FC ambao walipata pointi tatu na kuzawadiwa medali ya fedha, katoni ya bia ya Castle Lager na Sh 600,000.

Akizungumza baada ya bonanza hilo, meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli, aliwapongeza mabingwa hao kwa kutwaa ubingwa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*