googleAds

EYMAEL ASHTUKIA MCHEZO MCHAFU

NA WINFRIDA MTOI

KOCHA wa Yanga, Mbelgiji Luc Eymael, ameshtukia mchezo mchafu wanazofanyiwa washambuliaji wake,David Molinga na Bernard Morrison kwa kuwa ni hatari.

Molinga na Morrison ni washambuliaji tegemeo katika kikosi cha Yanga kwa kufunga mabao Ligi Kuu Tanzania Bara, inayoendeleza mzunguko wa pili.

Hata hivyo, Eymael amebaini mchezo mchafu kutokana na mabeki wa ligi hiyo, kuwawekea ulinzi makali ili wasifurukute mbele yao.

Lakini baya zaidi kumesababisha washambuliaji kushindwa kutimiza majukumu yao vizuri kutokana na kuchezewa rafu nyingi, ambazo zinaweza kuwaweka nje ya uwanja kwa muda mrefu, wakati timu ikihitaji matokeo bora ili waweze kukimbizana mbio za kuwania ubingwa.

Morrison kwa sasa anaonekana ni kivutio uwanjani kwa wapenzi wa timu hiyo, kutokana na uwezo wake wa kuchezea mpira, lakini Eymael amesema ameanza kukamiwa na mabeki wengi.

Eymael alisema kumekuwa na tabia ya  wachezaji wake kukamiwa na kufanyiwa rafu nyingi na wakati mwingine hata mwamuzi haoni tatizo hilo.

Kocha huyo alisema kutokana na sababu hiyo, atakuwa akiwatumia wachezaji tofauti ya wale walikaririwa na wapinzani ili kukwepa kusudi mbaya.

Yanga wanatarajia kukutana na Tanzania Prisons katika mchezo unaofuata wa Ligi Kuu, unataochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Yanga inashika nafasi ya tatu kutokana na pointi 38 baada ya kushuka dimbani mara 19, imeshinda mechi 12, sare tano na kupoteza tatu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*