Duh! Emery kikaangoni Arsenal

LONDON, England

KOCHA wa Arsenal, Unai Emery, anaweza kukalia kuti kavu ndani ya klabu hiyo kama atashindwa kufanikisha kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao ikiwa tayari msimu huu ametumia kiasi cha pauni milioni 152 kusajili wachezaji.

Huu ni msimu wa pili mfululizo Arsenal wanashiriki Ligi ya Europa jambo ambalo linawakera mabosi wa klabu hiyo na sasa kuamua kumpa kazi maalumu Emery aliyechukua mikoba ya Arsene Wenger.

Tayari, timu hiyo yenye maskani yake Uwanja wa Emirates, wapo nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kucheza michezo nane.

Mkuu wa Michezo wa Arsenal, Raul Sanllehi, alitoboa siri ya Emery raia wa Hispania kuwa atafukuzwa kama watashindwa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

“Malengo yetu siku zote ni makubwa, lazima tuyafikie japo kwa asilimia 80, naamini msimu huu tutafanikiwa kufanya vizuri na kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikishindikana Emery atakuwa kwenye wakati mgumu, labda atapoteza kazi yake, huwezi kujua,” alisema. 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*