googleAds

Deo Kanda kuwakimbiza mwanzo mwisho Lipuli

NA ZAINAB IDDY

MSHAMBULIAJI wa pembeni wa timu ya Simba, Deo Kanda, wanatarajiwa kuanza katika kikosi kitakachocheza kesho dhidi ya Lipuli kwenye Uwanja wa Samora.

Kanda alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza jeraha alilopata katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga uliochezwa Januari 4, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Simba wanatarajiwa kukutana na Lipuli ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara, baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa Jumanne iliyopita kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Kanda ambaye kwa muda mrefu ameshindwa kutimiza majuukumu yake uwanjani kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya ngoya aliyoyatapa wakati wa michuano ya Mapinduzi yaliofanyika Zanzibar.

Akizungumza na BINGWA jana akiwa njiani kwenda mkoani Iringa, Dakatari wa Simba, Yassin Gembe, alisema kwa sasa Deo yupo fiti na atakuwa miongoni  mwa wachezaji watakaoanza mchezo wa kesho dhidi ya Lipuli.

“Awali alikuwa aanze kucheza mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar kwa bahati mbaya haikuwezekana kutokana na jeraha lingine dogo mguuni, nashukuru yupo salaama,” alisema Gembe.

Alisema wachezaji wengine waliosafiri nao wako vizuri kiafya na kocha atakuwa na uamuzi wa kumtumia yeyote katika mchezo wa kesho.

Simba wanaongoza katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 53 baada ya kucheza michezo 21, wakishinda 17, sare mbili na kupoteza miwili.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*