googleAds

Chirwa ajifua kivyake Chamazi

NA TIMA SIKILO

MSHAMBULIAJIwa timu ya Azam, Obrey Chirwa, ameendelea kufanya mazoezi kivyake, licha ya wachezaji wenzake kuwa mapumzikoni.

Chirwa ambaye ni raia wa Zambia, amekuwa akifanya mazoezi kila siku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujiweka fiti zaidi.

Akizungumzia mchezaji huyo, kocha msaidizi wa timu hiyo, Idd Cheche, alisema nyota wao anatumia muda mwingi kujifua.

Cheche alisema pamoja na mchezaji huyo kumaliza mkataba wake, lakini ameamua kufanya mazoezi binafsi ili kutunza kiwango chake.

 “Ni mchezaji makini sana na anajua kutunza kiwango chake uwanjani, ” alisema.

Azam ilimaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, iliyomalizika hivi karibuni, lakini watashiriki Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kutwaa ubingwa wa AzamSports Federation Cup (ASFC).


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*