Category: Uncategorized

Deschamps hamtaki Benzema

PARIS, Ufaransa KOCHA wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps amethibitisha hatamwita mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema katika kikosi hicho. Benzema hayupo katika timu yake hiyo ya taifa tangu mwaka 2015, baada ya madai ya ubakaji pamoja na mchezaji mwenzake, Mathieu Valbuena. Hata hivyo Benzema ni mshambuliaji tegemeo wa Real Madrid, akiisaidia kubeba mataji likiwamo la Ligi ya […]

ZAA yaandaa michuano Gombani Pemba

NA IBRAHIM MAKAME, ZANZIBAR CHAMA cha Riadha Zanzibar (ZAA), kimeandaa michuano itakayofanyika Ijumaa wiki hii hadi Oktoba 23, mwaka huu, kwenye viwanja vya Gombani. Akizugumza na BINGWA visiwani hapa, Katibu mkuu wa ZAA, Suleiman Nyambui, alisema michuano hiyo itashirikisha wilaya zote za Zanzibar na Kisiwani Pemba. Nyambui alisema  maandalizi ya michuano hiyo imekamilika na kila wilaya inatakiwa kujitegemea baada kuandaa […]

Niite Boshen: Rich Mavoko alinilipa vizuri nimchore tattoo ya Simba

KARIBU msomaji wa Jiachie na Staa Wako inayokupa nafasi ya kuwauliza maswali watu maarufu unaowakubali katika tasnia ya burudani. Leo tupo na Bryson Peter maarufu kama Niite Boshen ambaye ni msanii wa kuchora aliyejikita katika kuchora michoro ya mwilini ‘tattoo’ kwa mastaa na watu wa kawaida. SWALI:  Fadhiri Mataruma wa Tabora anauliza ulianza lini uchoraji wa tattoo? Niite Boshen: Uchoraji […]

Wachezaji Canada washiriki uokozi

WACHEZAJI kutoka Canada wamesaidia katika shughuli za uokoaji mjini Kamaishi baada ya mchezo wa Kombe la Dunia dhidi ya Namibia iliyokuwa ichezwe jana kufutwa kwa ajili ya usalama. Takribani watu 18 wamepoteza maisha kutokana na mvua kubwa na Kimbunga Hagibs kilichoikumba sehemu kubwa ya Japan. Serikali ya Japan imetuma majeshi kuokoa maisha wa watu huku kukiwa na dakika moja ya […]

Osaka kuiwakilisha Japan Olimpiki

ANAYESHIKILIA namba mbili ubora wa dunia mchezo wa tenisi, Naomi Osaka, amesema ataiwakilisha Japan kwenye mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika mwakani jijini Tokyo licha ya kuwa na uraia wa Marekani. Osaka mwenye asili ya Haiti, alizaliwa Japan kabla ya kuhamia New York, Marekani akiwa na umri wa miaka mitatu. Akizungumza kupitia kituo cha televisheni cha NHK nchini Japan, mwanadada huyo alisema […]

Rohr akana tetesi zinazomkabili

LAGOS, Nigeria KOCHA wa timu ya taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’, Gernot Rohr, amegoma kuzungumza hatima yake ikiwamo kudai  Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) mshahara. Rohr amebakiza mkataba wa mkataba wa miaka miwili na Super Eagles unaotarajiwa kufika tamati 2022. Shirikisho hilo limekiri Mjerumani huyo anadai mshahara wa mwezi Septemba mwaka huu. “Siwezi kuzungumza kuhusu hili, nipo bize kuiandaa […]

Sporting Lisbon kumpa heshima Ronaldo

LISBON, Ureno NYOTA wa Juventus, Cristiano Ronaldo, jina lake litaandikwa katika uwanja wa klabu yake ya zamani ya Sporting Lisbon ikiwa ni sehemu ya heshima na kumuenzi. Heshima hiyo ni kutonaka na mambo makubwa ambayo ameyafanya kwa klabu hiyo akiwa mchezaji na pia kwa taifa zima la Ureno. Awali uwanja huo uliofanyiwa marekebisho uliandikwa jina la mkongwe wa timu hiyo, […]

Rio azidi kumuunga mkono Solskjaer

MANCHESTER, England BEKI wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand, anaamini utakuwa ujinga endapo bodi ya klabu hiyo itamtimua kocha anayekinoa kikosi hicho, Ole Gunnar Solskjaer. Tangu msimu umeanza, Man United imekusanya pointi tisa wakishuka uwanjani kucheza mechi nane za Ligi Kuu England. Imeripotiwa takwimu hizo ni mbovu kuwahi kutokea kwa miaka 30 Old Trafford, hata hivyo beki huyo wa zamani […]

Southgate awapa onyo wachezaji England

LONDON, England KOCHA wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate amewataka wachezaji wa kikosi hicho, kuongeza juhudi endapo wanataka kubeba taji la Kombe Mataifa ya Ulaya (Euro) mwakani. Kauli hiyo aliisema baada ya England kupokea kichapo cha mabao 2-1, dhidi ya Czech ukiwa ni mchezo wa kufuzu michuano hiyo. Southgate alikerwa na matokeo hayo ambayo England, ilikuwa wageni wa Czech […]