Category: michezo kimataifa

Dembele afungua njia kwa wanaomtaka

PARIS, Ufaransa  MSHAMBULIAJI wa Lyon, Moussa Dembele ametaka kurejea Ligi Kuu England, na kujiunga na timu yoyote itakayomuhitaji kwa mujibu wa ripoti. Timu hizo zilizotajwa ni Manchester United na Everton, ambazo zinamfuatilia kwa ukaribu mshambuliaji huyo. Itakumbukwa Dembele aliwahi kukipiga Fulham msimu wa 2012-2013 kabla ya kuondoka na kujiunga na Lyon. Dembele ameonyesha kiwango kizuri msimu huu huku akiwa amefunga […]

Kipa mkongwe Liverpool ampa tano Romero

MERSEYSIDE, Liverpool  KIPA wa zamani wa Liverpool, David James, anaamini uwezo wa kipa wa Manchester United, Sergio Romero, hauna tofauti na Alisson. Romero atasimama langoni kuchukua nafasi ya David de Gea ambaye anauguza majeruhi aliyopata akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Hispania. “De Gea ni namba moja bila shaka, lakini nikimwangalia Romero tangu alipojiunga Man United, amekuwa na […]

Berbatov ataka mashabiki wabaguzi wafungiwe maisha

SOFIA, Bulgaria  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Tottenham, Dimitar Berbatov, amewaponda mashabiki wa Bulgaria waliyoonyesha vitendo vya kibaguzi na kuitaka Shirikisho la Soka nchini humo (BFF) kuwafungia maisha kujihusisha na masuala ya soka. Kitendo cha mashabiki hao kuwaita nyani wachezaji weusi kutoka England, kimemkera na amekilaani. Tukio hilo limetokea wakati England ilipomenyana na Bulgaria katika mechi ya kufuzu michuano ya Kombe […]

Pochettino haendi popote

LONDON, England  KOCHA wa Tottenham, Mauricio Pochettino, anaamini wachezaji wake wote wapo nyuma yake na ataendelea kukinoa kikosi hicho bila yhofu. Kauli hiyo aliisema baada ya baadhi ya mastaa wa timu hiyo kumwalika chakula cha usiku katika moja ya mgahawa maarufu jijini London. “Kila mchezaji alinitumia ujumbe wa mwaliko, hii ni dalili nzuri sana, kujenga umoja na ushikirikano kwenye timu […]

El Clasico yapigwa kalenda Hispania

CATALUNYA, Hispania HALI ya usalama imezidi kuwa mbaya katika Mji wa Catalunya nchini Hispania, baada ya wakazi wao kufanya maandamano ya kisiasa yaliyopelekea mchezo wa Barcelona na Real Madrid kusogezwa mbele.  Shirikisho la Soka Hispania (RFEF) lilifikia makubaliano ya kuahirishwa kwa mchezo huo mkubwa nchini humo kutokana na maandamano hayo ambayo yametibua hali ya amani. Hata hivyo, taarifa za awali […]

CHONGENI TU… Bosi Man United amkingia kifua Solskjaer, kufanya vibaya sio ishu

MANCHESTER, England BILA shaka habari za kocha wa zamani wa Juventus, Massimilliano Allegri kuhusishwa na Manchester United si ngeni miongoni mwa wapenzi wa soka, lakini kupitia kwa Mtendaji msaidizi wa klabu hiyo, Ed Woodward, amekanusha taarifa hizo na kudai bado wanamwamini Ole Gunnar Solskjaer. Manchester United wapo nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu England, pointi 15 nyuma ya […]

Kinda Barcelona haendi popote

CATALUNYA, Hispania MSHAMBULIAJI kinda wa timu ya Barcelona, Ansu Fati, yuko mbioni kuongeza mkataba wa muda mrefu wenye thamani ya pauni milioni 88 (Tsh bil.254). Barcelona inataka kumpatia mkataba huo mnono kinda wao huyo, baada ya kuvutiwa na kiwango chake tangu ilipompandisha kikosi cha kwanza. Fati alianza kufuatiliwa na klabu nyingine kubwa Barani Ulaya, lakini Barca inataka kumhakikishia muda mwingi […]

RUGBY

Wales sasa kuivaa Ufaransa robo fainali WALES walipambana kupata pointi za bonasi dhidi ya Uruguay na kushinda 35-13 sasa watavaana na Ufaransa katika mchezo wa robo fainali. Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu kwa Wales ambao waliongoza kwa taabu 7-6 kupitia kwa Nicky Smith huku wakifanya makosa mengi hususan namna ya ushikaji mpira. Josh Adams aliwaongezea uongozi Wales lakini German Kessler […]