Category: Habari

Makame, Balama tema mate chini

NA MAREGES NYAMAKA KIWANGO cha nyota wawili wa Yanga, Abdulazizi Makame sambamba na Balama Mapinduzi katika mchezo wao jana Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya Zesco kilikuwa bora zaidi kuliko mchezaji yeyote wa timu hiyo. Makame hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika alikuwa amepiga pasi sahihi 69 zote zikimfikia mlengwa, na kutengeneza […]

Katibu Mkuu Yanga aundiwa zengwe

NA MWANDISHI WETU BAADA ya taarifa kuvuja kwamba uongozi wa Yanga umemteua mwanachama wake, David Ruhango, kuwa Katibu Mkuu, tayari hatua hiyo imeanza kuundiwa zengwe. Habari zilizoenea katika mitandao ya kijamii zilidai kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokaa hivi karibuni kilipitisha majina matatu ya David Ruhago kuwa Katibu Mkuu, Hassan Bumbuli kuwa Ofisa Habari na Antonio Nugazi kuwa Ofisa Mhamasishaji […]

AZAM FC WAIVAA ZIMBABWE KIBAHARIA

NA JESSCA NANGAWE WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Azam FC, leo itatupa karata yake ya kwanza mbele ya Triangle United ya Zimbabwe katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi. Baada ya mchezo huo timu hizo zitarudiana tena baada ya wiki mbili katika mchezo utakaoipigwa jiji la Harare, nchini Zimbabwe. Akizungumzia mchezo huo, kocha […]

KIBOKO YA YANGA ARUDISHWA SIMBA

NA MWANDISHI WETU SAA chache baada ya Mwenyekiti wa Simba, Swed Mkwabi, kutangaza kujiuzulu, taarifa mpya kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema aliyewahi kuwa Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdalah ‘Try Again’, ndiye anayetarajiwa kukaimu nafasi hiyo. ‘Try Again’ ndiye aliyekaimu nafasi ya aliyekuwa Rais wa Simba, Evans Aveva, ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya madai ya kutakatisha pesa, […]

AUSSEMS AKATAA MABAO KIDUCHU

NA MWANDISHI WETU SIMBA ilianza Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania, kisha juzi Ijumaa ikapata ushindi mwingine wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, sasa unaambiwa kocha mkuu, Patrick Aussems, amekataa ushindi wa mabao machache. Aussems muda mfupi baada ya mchezo wa juzi, alisema anashukuru timu yake kupata pointi hizo tatu […]

Akina Bukungu wawatoa ofisini mabosi KMC

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa KMC umetoka ofisini na kwenda kuomba msaada kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lifuatilie uhamisho wa wachezaji wao wawili wa kigeni, Besala Bukungu raia DR Congo na Mnyarwanda Jeans-Baptise Mugiraneza. Wachezaji hao waliosajiliwa dirisha la Ligi Kuu Tanzania Bara la Juni hadi Julai, mwaka huu, wameshindwa kuitumia timu yao mpya kutokana na kucheleweshwa uhamisho na […]

Mbonde aanza mazoezi mepesi

NA ASHA KIGUNDULA BEKI wa zamani wa Simba, Salum Mbonde, ameanza mazoezi mepesi, baada ya kupona jeraha lililokuwa linamsumbua kuanzia msimu wa 2017/2018 wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Akizungumza na BINGWA jana, Mbonde alisema anafanya mazoezi chini ya uangalizi wa daktari wa tiba za michezo nchini, Gilbert Kigadya. Alisema kwa sasa ana wiki mbili tangu aanze mazoezi mepesi huku akisubiria […]

Ndayiragije awatoa hofu Azam

NA TIMA SIKILO KOCHA wa Azam, Etienne Ndayiragije, amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Triangle Unitedya Zimbabwe utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Akizungumza na BINGWA jana, Ndayiragije alisema timu yake itafanya vizuri Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa. Ndayiragije alisema wamejipanga kufanya vizuri michuano […]