Aubameyang aomba radhi

LONDOND, England
FOWADI wa Arsenal, Pierre Emerick Aubameyang, ameomba radhi mashabiki kwa kadi nyekundu, aliyopewa wikiendi iliopita.

Kitendo hicho ni baada ya kumchezea rafu mbaya mchezaji wa Crystal Palace, Max Meyer timu hizo zilipokutana kwenye mechi ya Ligi Kuu England, na kufungiwa mechi tatu.

“Haikuwa kusudio langu kucheza rafu ile, nina imani Max atapona, lengo langu ni kuuchukua mpira, kilichotokea ni bahati mbaya, “ alisema Aubameyang.

Arsenal ilimkosa fowadi juzi iliposhuka dimbani kucheza na Sheffield United, Arsenal ikiambulia sare ya bao 1-1.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*