Sarri kuanza na Giroud mapema

LONDON, England

TIMU ya Chelsea imepanga kumwongezea mkataba wa mwaka mmoja straika wa kikosi hicho, Olivier Giroud, ambaye alitajwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu kwa kukosa nafasi ya kucheza.

Lakini kocha wa kikosi hicho, Maurizio Sarri, ameuambia uongozi wa timu hiyo ufanye haraka kumpa mkataba straika huyo ambaye amepachika mabao 10 katika michuano ya Ligi ya Europa.

Hata hivyo, Chelsea walifungiwa na Shirikisho la Soka Duniani, Fifa, kwa kukiuka sheria za usajili huku rufaa ya vigogo hao wa England ikitupiliwa mbali.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*