Ramsey aibukia Italia fasta

TURIN, Italia

MAPEMA tu Aaron Ramsey alisafiri mpaka nchini Italia kuangalia mchezo wa mwisho wa ligi hiyo kati ya Juventus na Atalanta uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Kiungo huyo raia wa Wales, atajiunga na kikosi cha Juventus msimu ujao akiwa mchezaji huru kutokea Arsenal ambako alikaa miaka 11.

Ramsey ambaye alicheza michezo zaidi ya 350 ndani ya kikosi cha Arsenal, aliisaidia timu hiyo kushinda mataji mawili ya Kombe la FA.

Tayari msimu wake umemalizika ndani ya Arsenal baada ya kuumia goti huku kikosi hicho cha Unai Emery kikitarajiwa kucheza mchezo wa fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Chelsea.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*