Pepe aibeba tuzo ya Afrika kule Ufaransa

PARIS, Ufaransa

WINGA raia wa Ivory Coast anayeichezea Lille, Nicholas Pepe, ameinyakua tuzo ya Mwafrika Bora kwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Ufaransa ‘Ligue 1’.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, aliibuka kidedea kwa kuwazima Whabi Khazri wa Tunisia (Saint-Etienne) na raia wa Senegal, Ismaila Sarr (Rennes).

Pepe anakuwa mwanasoka wa tatu kutoka Ivory Coast kuipeleka nyumbani tuzo hiyo kwa mabao 22 na asisti 12.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*