SMG amtabiria makubwa Molinga

NA WINFRIDA MTOI SIKU chache alizokaa na straika mpya wa Yanga, David Molinga, kocha wa timu ya vijana wa Wanajangwani hao, Said Maulid ‘SMG’, amesema mchezaji huyo akipewa muda, atafanya mambo makubwa. SMG aliachiwa Molinga na wachezaji wengine wiki iliyopita kuwasimamia katika mazoezi, wakati Yanga ilipokuwa Botswana kuvaana na Township Rollers, ukiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika walioshinda […]

Manula ambariki Kaseja Taifa Stars

NA MWAMVITA MTANDA KIPA wa Simba, Aishi Manula, amesema hana kinyongo kutokana na kutemwa katika kikosi cha Taifa Stars na badala yake amebariki Juma Kaseja kubeba jahazi. Manula ametemwa katika kikosi hicho kinachojiandaa kucheza na Sudan keshokutwa katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa Ligi ya Ndani (Chan), utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. […]

Aveva, Kaburu warudi uraiani

NA KULWA MZEE RAIS wa zamni wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’, wamepata dhamana na shtaka la kutakatisha fedha limeondolewa, baada ya mahakama kuwaona hawana kesi ya kujibu. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, ilifikia uamuzi huo jana, ikiwa ni zaidi ya miaka miwili wakati inatoa uamuzi kama washtakiwa […]

Makambo amaliza mjadala wa Molinga

NA MWAMVITA MTANDA HERITIER Makambo aliyejizolea maujiko Yanga kutokana na umahiri wake wa kucheka na nyavu, amefunga mjadala juu ya wasiwasi walionao mashabiki wa klabu hiyo kuhusiana na kiwango cha straika wao mpya David Molinga. Molinga alitua Yanga dakika za mwisho za dirisha la usajili uliopita, akiletwa Jangwani ili kutatua tatizo la mabao, baada ya wachezaji waliosajiliwa mapema kipindi hicho, […]

KAGERE BADO KIZA KINENE SIMBA

NA WINFRIDA MTOI HALI ya uchovu ya straika wa Simba, Meddie Kagere, imemshtua Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Patrick Aussems baada ya kuanza kuchukua tahadhari kuelekea mechi dhidi ya Kagera Sugar. Wekundu wa Msimbazi hao, wanatarajia kukutana na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Septemba 26, mwaka huu, Uwanja wa Kaitaba Kagera, mjini Bukoba. Kagere tangu […]

Mrembo amfungia kazi Balinya

NA MWAMVITA MTANDA MREMBO Winfrida Shonde ameamua kuwafungia kazi wachezaji wa kigeni wa Yanga, lakini si kwa vile wengi wanavyoweza kufikiria, bali ni katika kuwafanya waweze kutekeleza ipasavyo majukumu yao yaliyowaleta hapa nchini. Winfrida ambaye ni mwanasaikolojia, amekuwa akiwajenga wachezaji hao kisaikolojia kuwawezesha kuzoea mazingira ya hapa nchini, soka la Tanzania na klabu hiyo kwa ujumla, baada ya uongozi wa […]

Bumbuli, Nugaz rasmi Yanga

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Klabu ya Yanga, umemtangaza rasmi, Hassan Bumbuli kuwa Ofisa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, huku Antonio Nugaz akiwa Ofisa Mhamasishaji. Nafasi aliyopewa Bumbuli ilikuwa ikishikiliwa na Dismas Ten ambaye kwa sasa ni Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, lakini Ofisa Mhamasishaji ni mpya klabuni hapo. Katika taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga jana, Mwenyekiti wa […]

Selekta Davizo kutangaza utamaduni

NA PENDO HAMISI (TUDARco) KUTOKA lebo ya Bunduki Music, mkali wa muziki nchini, Selekta Davizo, amesema wimbo wake mpya Ngoma Hii yenye vionjo vya Kiafrika ni miongoni mwa mipango yake ya kutangaza utamaduni wa Afrika. Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Selekta aliyewahi kutamba na nyimbo kama Champion na Uzuri Wako alisema anashukuru mapokezi ya wimbo huo yamekuwa mazuri kutokana […]

Samatta ‘Poppa’ alivyojitosa takwimu za kiume usiku wa Uefa 2019-20

LONDON, England USIKU wa juzi, ulikuwa mtamu kwa mashabiki wa soka la Ulaya pale hatua ya makundi ya Ligi Mabingwa ilipoanza, mechi kadhaa zikichezwa, kabla ya nyingine kuendelea usiku wa kuamkia jana. Huenda ulipitwa na takwimu mbalimbali zilizowekwa, hivyo makala haya yanakuibulia rekodi zilizowekwa, zilizovunjwa na kuendelezwa usiku huo wa Jumanne ya wiki hii. Inter 1-1 Slavia Praha Haikushangaza kuona […]