Zidane: Simtaki Neymar wala Mbappe

MADRID, Hispania

ZINEDINE Zidane hakubaliani na harakati za Real Madrid chini ya Rais, Florentino Perez, kuzisaka saini za mastaa wa PSG, Neymar na Kylian Mbappe.

Huku uongozi wa Madrid ukiamini safu yake ya ushambuliaji inahitaji kuongezewa nguvu, Zidane aliibuka na kumsifia Karim Benzema ikiwa ni kuua dili la nyota hao.

Madrid wametajwa kuandaa mpunga wa maana kuwasajili Neymar na Mbappe pindi tu dirisha kubwa la usajili la majira ya kiangazi litakapofunguliwa.

Inaelezwa kuwa hata atakapowakosa wawili hao, Rais Perez atajaribu kumsajili Julian Draxler wa PSG ambaye usajili wake utagharimu euro milioni 45 tu.

Hata hivyo, kama ilivyo kwa Neymar na Mbappe, hata staa huyo raia wa Ujerumani hatakiwi na Zidane anayeamini Ulaya kuna viungo wengi waliomzidi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*