ZIDANE ANAONDOKA MADRID NA REKODI HIZI

MADRID, Hispania


JUZI, Zinedine Zidane aliushangaza ulimwengu wa soka kwa uamuzi wake wa kung’atuka katika benchi la ufundi la Real Madrid.

Taarifa hiyo inakuja zikiwa ni siku tano pekee zimepita tangu kiungo huyo wa zamani wa Madrid na timu ya Taifa ya Ufaransa alipoipa timu hiyo taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mjini Kive, Ukraine.

Licha ya kwamba si alizozisema, wachambuzi wa soka wameibua sababu tatu za Mfaransa huyo kuondoka ‘fasta’ Madrid.

Kwanza, wanaamini ‘Zizou’ anataka kutimka wakati huu kwa kuwa atabaki kwa muda mrefu katika historia ya timu hiyo, akiwa ndiye kocha pekee aliyeipa mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Pili, ipo dhana kuwa ameamua kuondoka ili kusaka changamoto mpya, ikizingatiwa kuwa Madrid ni klabu aliyokaa nayo kwa muda mrefu tangu akiwa mchezaji.

Tatu, inaamini kuwa licha ya vikombe tisa alivyowapa, haamini kuwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuifanya timu hiyo kucheza soka la kuvutia, hoja ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikijengwa na wakosoaji wake wanaosema hana mbinu.

Kwa habari zaidi pata nakala yako la gazeti la BINGWA hapo juu


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*