googleAds

Zanzibar yaanza kwa sare Chalenji

NA MWANDISHI WETU

TIMU ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, imebanwa baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Sudan katika mchezo wa Kundi B wa michuano ya Kombe la Chalenji uliochezwa jana, kwenye Uwanja wa KCCA, jijini Kampala, Uganda.

Michuano hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), ilianza juzi.

Katika mchezo huo wa jana, timu ya Zanzibar Heroes walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 54, lililofungwa na Makame Hamisi Mussa aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Awesu Awesu.

Zanzibar Heroes iliyoonesha kucheza soka nzuri, ilishindwa kulinda bao hilo, baada ya Sudan kusawazisha dakika ya 89 kupitia kwa Montasir Othmani kwa shuti kali.

Hata hivyo, Zanzibar Heroes walijikuta wacheza pungufu uwanjani baada ya Ahamada Ibrahim kuoneshwa kadi nyekundi iliyotokana na kadi mbili za njano.

Baada ya mchezo huo, Zanzibar Heroes wanajiandaa kucheza na Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ kesho jijini Kampala.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*