googleAds

ZAHERA AFICHUA MAPYA YA AJIB

 NA TIMA SIKILO


 

WAKATI mashabiki wa soka nchini wakiendelea kulimwagia sifa bao la ‘kideo’ lililofungwa na Ibrahim Ajib wa Yanga Jumapili iliyopita, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, amefichua mapya yanayofanywa na nyota huyo mazoezini, akiamini hakuna mchezaji yeyote anayeyaweza.

Ikiwa timu yake inaongoza kwa bao 1-0 hadi dakika ya 90, Ajib aliupata mpira uliookolewa na

mabeki wa Ndanda FC na kujikunja na kupiga ‘tik-tak’ bab kubwa na mpira kugonga mwamba wa juu kabla ya kutinga nyavuni.

Bao hilo ndilo lililoihakikishia Yanga ushindi katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kuondoka uwanjani na pointi zote tatu mbele ya wapinzani wao hao kutoka Mwanza.

Baada ya mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mashabiki wa Yanga na wengineo walikuwa wakilizungumzia bao hilo la Ajib, wakilipa nafasi ya

kuwa katika kinyang’anyiro cha bao bora la msimu.

Akizungumza na BINGWA jana, Zahera alisema alichokifanya mchezaji huyo kwake si kipya, kwani amekuwa akionyesha vitu adimu na vya kuvutia katika mazoezi

yao, kuanzia walipokuwa kambini Morogoro hadi jijini Dar es Salaam.

Alisema kutokana na akili aliyonayo Ajib, ana uwezo wa kufanya matukio makubwa zaidi uwanjani, akiwataka mashabiki wa Yanga kutarajia mambo matamu zaidi kutoka kwa mkali

wao huyo.
“Eeeh! Ni mara ya kwanza

Watanzania kuona kitu kama kile kwa Ajib? Mimi hainishangazi, kwasababu nimeshaona akifanya hivyo mara nyingi, pia kutokana na akili yake, ana uwezo wa kufanya kitendo kikubwa zaidi ya kile,” alisema Zahera.

Alisisitiza ameshakaa na mchezaji huyo na kumshauri jinsi ya kuwa moto zaidi, akiamini hakuna mchezaji hapa nchini anayemfikia kwa ‘maufundi’ awapo uwanjani.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*