googleAds

Zahera unataka kuitoa Zesco? Msikie huyu

NA TIMA SIKILO

KUELEKEA mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika dhidi ya Zesco United ya Zambia utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga wamepewa ushauri wa nini wafanye ili wasonge mbele.

Mchezo huo ni wa raundi ya kwanza na kwamba timu itakayopita, itatinga hatua ya makundi ya michuano hiyo, wakati ile itakayotolewa, itaangukiwa Kombe la Shirikisho Afrika mtoano.

Mmoja wa wachezaji wa soka wa Zambia, Andrew Kwiliko, ameliambia BINGWA kuwa Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, anatakiwa kuchukua tahadhari kwa wachezaji watatu wa Zesco na kwamba akifanikiwa kuwadhibiti, Wanajangwani hao njia nyeupe hatua ya makundi.

Mchezaji huyo anayekipiga katika kikosi cha Green Eagles ya Zambia, amesema kuwa japo kikosi cha Zesco kipo vizuri kuanzia mwalimu hadi wachezaji, lakini wapo iwapo Yanga itawakamata nyota wake, Jesse Were na John Ching’andu na kiungo Anthony Akumu, wapinzani wao hao hawatafurukuta.

“Mimi naona hao watatu wanauwezo mkubwa sana, ukizingatia Jesse Were ndiye aliyeongoza kwa mabao msimu uliopita, ni mchezaji wa hatari na muda wote anachokifikiria ni kufunga tu,” alisema.

Alisema wachezaji hao wana uzoefu mkubwa na ligi za ndani na hata michuano ya kimataifa, hivyo Yanga ni vema wakawaangalia kwa makini na kutowapa kabisa nafasi ya kufanya watakalo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*