googleAds

Zahera ataja bei ya ‘kipensi’ chake

SISCA MACHABA (TUDARCo) NA WINFRIDA MTOI

BAADA ya kukumbana na adhabu kutokana na mavazi yake, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameweka bayana bei ya ‘mapigo’ yake hayo ambayo ni Euro 900, zaidi ya sh. milioni 2 za Kitanzania.

Hivi karibuni, Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (TPLB), ilimpiga  Zahera faini ya sh. 500,000, kwa kosa la kuvaa mavazi  yasiyo nadhifu na heshima wakati wa mechi yao na Ruvu Shooting iliyochezwa Agosti 28, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na Yanga kufungwa bao 1-0.

Akizungumzia mavazi hayo jana, Zahera alisema anashangaa kuona amepigwa faini na mavazi ambayo yeye anayanunua kwa bei mbaya, kutokana na kuyapenda.

Alisema huwa anavaa nguo kulingana na hali ya hewa, kama ni joto ni zile zinazomfanya ajisikie vizuri kipindi hicho, wakati wa baridi pia ana mavazi anayopenda.

“Nina nguo nyingi sana na nazinunua kwa gharama kubwa, mfano zile walizonipiga nazo faini ambazo napendelea, kaptula na fulana nimenunua kila moja Euro 400 na kofia Euro 100.

“Ujue ninavaa nguo kulingana na mazingira na hali ya hewa, hapa Dar es Salaam ni joto ndiyo sababu navaa kaptula, lakini kipindi cha baridi huwezi kuniona vile,” alisema Zahera.

Hata hivyo, katika mazoezini ya jana, kocha huyo alionekana akiwa amevaa suluali na fulana zenye nembo ya Yanga.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*