Zahera alia na waamuzi 

Lulu Ringo, Dar es salaam.

 Kocha mkuu wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera amewaomba viongozi wa mpira nchini kuwa makini na waamuzi wanaochezesha mechi za Ligi Kuu kwani wanaharibu maana ya mpira.

Akizungumza na Bingwa Online Zahera amesema hakuridhishwa na maamuzi ya mwamuzi Meshack Suda, aliyechezesha mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons jijini Mbeya mchezo uliomalizika kwa Yanga kushinda magoli matatu kwa moja.

“Nawaomba viongozi wa mpira kuwa makini na waamuzi wanaocheza michezo ya Ligi Kuu, mnapaswa kujua hizi mechi zinaonekana hadi nje ya nchi kama, Kenya, Rwanda na Congo wote hawa wanajionea yale yana yatokea uwanjani.

“Nimepigiwa simu kutoka Rwanda, kuna watu wanauliza mchezo wetu na Prisons mbona umekuwa na maamuzi yasio sawa, nimeshuhudia maamuzi yasio ya kizalendo lakini cha kushangaza waamuzi hawapati adhabu yoyote,” amesema Zahera.

Katika mchezo huo muamuzi alitoa adhabu ya penalti kwa Yanga dakika ya 43 baada Andrew Vicent kumchezea rafu Salum Kimenya wa Prisons maamuzi yaliyoleta mtafaruku.

Aidha dakika ya 50 refa huyo alitoa adhabu ya kadi mbili nyekundu moja ilikwenda mchezaji wa yanga Mrisho Ngasa kwa kumpiga kichwa Hasan Kapatalata na  nyingine alipewa Laurian Mpalile baada ya kurejesha kwa Ngasa kile alicho kifanya kwa mchezaji mwenzie.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*