Young: Mambo mazuri yatakuja tu

MANCHESTER, England 

BEKI wa Manchester United, Ashley Young, ana imani timu hiyo itarudi kwenye ubora wake, hivyo mashabiki wasipaniki kutokana na kiwango chao kibovu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Young alisisitiza anafahamu timu hiyo inapoelekea kwasasa.

“Vijana wanafanya mazoezi kwa bidii, matokeo mazuri ni kwa timu, kila mchezaji anafahamu hilo, ushindi huleta morali ya kusonga mbele na kufanya vizuri,” alisema.

Man United imeanza msimu kwa kusuasua na imepambana kuhakikisha wanabaki ‘Top Four’ ikiwamo kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Previous Article

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*