googleAds

YONDANI AJA JUU YANGA

 NA HUSSEIN OMAR              |               


 

BEKI wa Yanga, Kelvin Yondani, amethibitisha kuwa linapokuja suala la kusaka ushindi uwanjani huwa hataki masihara hata kidogo, baada ya juzi wakati wa mchezo dhidi ya Mbao FC kuonekana kuwajia juu wenzake kila walipofanya makosa ya kizembe.

Pambano hilo la Ligi Kuu Tanzania Bara liliishia kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na hivyo kuchanja mbuga katika harakati zao za kutaka kulirejesha tena Jangwani taji la ubingwa ambalo msimu uliopita walilipoteza kwa Simba.

Kwenye mtanange huo wa juzi, kipa wa Yanga, Benno Kakolanya, kama kawaida yake alisimama vyema golini kabla ya kuumia dakika ya 59 na nafasi yake kuchukuliwa na Claus Kindoki ambaye naye hakuwaangusha mashabiki wa timu hiyo.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la BINGWA.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*