YEMI ALADE AFICHUA KUBAGULIWA UINGEREZA

LAGOS, Nigeria


BIBIYE Yemi Alade amesema alifanyiwa vitendo vya ubaguzi wakati akiwa kwenye ndege akielekea Uingereza.

Msanii huyo wa muziki wa Afro-pop, hakuwa tayari kuliweka hadharani jina la ndege hiyo alipokuwa akisimulia mkasa huo kupitia akaunti yake ya mtandao wa Instagram.

Alisema wakati alipokuwa ameuchapa usingizi kidogo, alishtuka kuona mmoja kati ya wahudumu akimvuta mguu kwa lengo la kumwamsha, jambo ambalo Yemi anaamini asingefanyiwa abiria wa Kizungu.

Hivi karibuni, mwanadada huyo alikuwa gumzo katika mitandao ya kijamii, baada ya mahojiano yake na kituo cha redio cha Hot 98.3, ambapo alisema Nigeria haina staa namba moja licha ya Davido na Wizkid kuonekana kuwa ndio wanaoliburuza soko la muziki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*