YCEE APONDA BEI KALI JEZI NIGERIA

LAGOS, Nigeria


 

MWANAMUZIKI Ycee amewakingia kifua mashabiki wa kandanda wanaonunua jezi feki za timu ya Taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’, akisema ni kutokana na bei kali ya zile halisi (original).

Jezi moja halisi itakayotumiwa na Super Eagles katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu inapatikana kwa Naira 41,000 (Sh 257,110 za Tanzania).

Bei hiyo ilitangazwa siku chache zilizopita na kuzua taharuki kubwa kwa mashabiki wa soka, wengi wao wakisema ni ngumu kwa wananchi wa kawaida kuimudu.

Naye Ycee alikuwa upande wao akiandika katika akaunti yake ya mtandao wa twitter: “…nafikiri si sahihi kuwakosoa wanaovaa jezi feki kwa kuwa wengi wetu wananchi hatuwezi kumudu Naira 41,000 kununua jezi moja.”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*