Yaya Toure bado yupo sana

BEIJING, China 

KIUNGO wa zamani wa Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast, Yaya Toure, amejiunga na klabu ya Qingdao Huanghai ya Ligi Kuu China. 

Mwanandinga huyo mwenye umri wa miaka 36, anatarajiwa kushuka dimbani wikiendi hii, kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na klabu hiyo dhidi ya Zhejiang Greentown.

Toure, amekuwa nje ya dimba tangu Desemba mwaka jana, alipokuwa akikipiga katika klabu ya Olympiacos akiwa amedumu kwa muda miezi mitatu.

Awali, mkongwe huyo alitangaza kuwa atatundika daruga, lakini hali imekuwa tofauti kwa mchezaji huyo aliyeitumikia Manchester City kwa miaka tisa.

Toure aliwahi kukipiga katika klabu nyingine kadhaa, zikiwamo Monaco na Barcelona.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*