googleAds

Yanga yatamba iko kamili kuikabili Zesco

Richard Deo, Dar es Salaam

Kikosi cha Timu ya Yanga SC, kimesema kipo kamili kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Zesco United ya nchini Zambia utakaopigwa kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Noeli Mwandila wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Septemba 13.

“Kikosi kiko vizuri na tunaendelea kujiandaa baada ya kurejea kutoka mwanza tulikocheza michezo ya kirafiki dhidi ya Toto Africa na Pamba na kupata matokeo ya ushindi Kwa mchezo mmoja na sare mchezo mmoja,” amesema.

Wanajangwani hao watashuka dimbani kesho kupambana na Zesco Katika mchezo wa raundi ya Pili wa ligi ya mabingwa barani Africa, baada ya mchezo wa kwako kuwatoa Township Rollors Kwa jumla ya Mabao 2-1.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*