YANGA YAPEWA MCHONGO

NA ZAITUNI KIBWANA


 

YANGA wametakiwa kutofanya kosa la kutumia ipasavyo fursa ya kucheza mechi 11 mfululizo za nyumbani kwa kuhakikisha wanashinda zote na hivyo kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mechi hizo zitapigwa kwenye viwanja vya Taifa na Uhuru, Dar es Salaam, huku watani wao wa jadi, Simba, wakitoka nje ya jiji hilo, kesho wakitarajiwa kuivaa Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Akizungumza na BINGWA jana, nahodha wa zamani wa timu hiyo, Ally Mayay, alisema Yanga mara zote wanazotangaza ubingwa mapema, huwa wanapata pointi nyingi katika mechi za nyumbani tofauti na mechi za ugenini, hivyo Wanajangwani hao wanapaswa kutofanya mzaha na kuhakikisha wanashinda michezo hiyo.

“Siku zote Yanga na Simba huwa wanatangaza ubingwa baada ya kupata pointi nyingi katika michezo yao ya nyumbani, hivyo Yanga wanapaswa …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la BINGWA.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*