googleAds

YANGA WATEGUA MITEGO

 

Katika hatua nyingine, Yanga wameitegua mitego yote waliyotegewa na Simba kwa kuongeza ulinzi kikosini mwao kukwepa hujuma zozote zitakazoelekezwa kwa wachezaji wao.

Kama Simba walidhani kwa kubaki Dar es Salaam wanaweza kutega mitego ya kuinasa Yanga, imekula kwao kwani tayari watani wao hao wa jadi wameweka mambo sawa kuhakikisha hakuna kinachoharibika.

Yanga wanafahamu kuwa pambano la watani siku zote linakuwa na hila kadha wa kadha za nje ya uwanja, hivyo wameona ni vyema kujipanga kwa kila namna ili mshindi apatikane kihalali.

Hata hivyo, kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, timu hizo zinapokutana Septemba huwa hazina matokeo ya kutisha zaidi ya sare.

Katika mechi 10 ambazo timu hizo zimewahi kukutana tangu mwaka 1981, kila moja imeshinda mara tatu tu huku mechi nyingi zikitoka sare.

Habari hii imeandaliwa na ZAITUNI KIBWANA, SAADA SALIM, HUSSEIN OMAR NA AYOUB HINJO


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*